John 8:50-54

50 aLakini mimi sitafuti utukufu wangu mwenyewe, bali yuko anayetaka kunitukuza, naye ndiye mwamuzi. 51 bAmin, amin nawaambia, mtu yeyote akilitii neno langu hataona mauti milele.”

52 cNdipo Wayahudi wakamwambia, “Sasa tumejua kwamba una pepo mchafu. Ikiwa Ibrahimu alikufa na vivyo hivyo manabii, nawe unasema, ‘Mtu akitii neno langu hatakufa milele.’ 53 dJe, wewe ni mkuu kuliko baba yetu Ibrahimu ambaye alikufa na manabii ambao nao pia walikufa? Hivi wewe unajifanya kuwa nani?”

54 eIsa akawajibu, “Kama nikijitukuza utukufu wangu hauna maana. Baba yangu, huyo ambaye ninyi mnadai kuwa ni Mungu wenu, ndiye anitukuzaye mimi.
Copyright information for SwhKC